FINANCIAL INCLUSION > GROUP BANKING
M-KOBA
TPB Bank kwa kushirikiana Vodacaom tunatarajia kuzindua huduma ya Akaunti za vinkundi inayoitwa M-KOBA hudumu hii ni mahususi katika kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa Vikundi, kuweka uwazi ndani ya vikundi wapokuwa wanafanya shughuli zao na Usalama wa kifedha ndani ya vikundi.
Kwahiyo ili mwanakikundi au mwanajamii aweze kupata huduma hii ni lazima kwanza awe na laini ya VODA na pia awe amijisajili na huduma ya M-Pesa.
Huduma hii inapatikana katika M-PESA Menu:
Hivyo basi, pindi mwanakikundi/mwanajamii hatahitaji kupata huduma hii itabidi kwanza aingie kwenye Mpesa Menu akishaingia itabidi haende kwenye huduma za kibenki, Kisha M-KOBA.
Naomba sote kwa pamoja tushirikiane katika kuiuza bidhaa hii hadimu na ya aina yake sokoni.
M-KOBA
Vodacom kwa ushirikianona TBP Bank inawaletea wateja wake wote huduma mpya ya M-KOBA hii ni huduma mahususi kwa vikundi vidogo vidogo M-KOBA na vicoba kwa ajili ya kutunza fedha, mikopo, riba na mambo mengine yote yanayofanyika kwenye vikundi hivi.
Huduma hii imeleta: usalama wa fedha za wanakikundi, uwazi na urahisi kwasababu shughuli zote zinafanyika kidigitali.
Wanakikundi wanaweza kujiandikisha kwenye huduma hii kupitia menu ya M-Pesa *150*00# kisha chagua Huduma za kifedha halafu chagua M-KOBA
Kuna akaunti mbili katika M-KOBA
· Marafiki/Familia
· VICOBA/VSLA
Marafiki/Familia
Hii ni akaunti maususi kwa vikundi vidogo inaweza kuwa familia ama marafiki ambao wamekusudia kuchanga fedha na baadae kugawana baada ya muda Fulani.
Mfano: UPATU, Harusi.
VICOBA/VSLA
Hii ni akaunti maususi kwa ajili ya vikundi vyenye upana mkubwa wa wanachama na vilivyo na mfumo wa kuuza na kununua hisa, kuweka akiba, Michango ya Kijamii na Kupeana Mikopo. Vikundi hivi ni vile vihusishavyo VICOBA na VSLA.
Vigezo vya kufungua Akaunti ya Kikundi ya M-KOBA:
Kikundi cha M-KOBA kitatakiwa kuwa na wanachama wasiopungua watano.
Ili kutengeneza akaunti ya M-KOBA Kila kikundi kinapaswa kuwa na viongozi watatu.
Katika akaunti hii ya M-KOBA kutakua na wahidhinishaji watano ambapo kati yao kutakua na Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na Wanachama Wawili Lengwa.
Mwenyekiti huyu ndie kiongozi na admin wa kikundi, Mwenyekiti atakua na mamlaka ya kuongeza mwanachama na kumpa majukumu na vilevile yeye ndio mtu wa mwisho kuthibitisha kutuma fedha kwa mwanachama wa kikundi.
Na pia kutakua na Katibu ambae ataongezwa na mwenyekiti na yeye ndo atakae anaanzisha malipo yote M-KOBA na mikopo itolewayo kwa wanachama wa kikundi.
Na vilevile atakuwepo Mwekahazina, pia ataongezwa na mweneyekiti na kazi yake itakua ni kuthibitisha malipo na mikopo itolewayo kwa wanachama wa kikundi.
Ili kutoa pesa kutoka kwenye akaunti ya Kikundi kwenda kwa mwanachama wa kikundi viongozi wa kikundi wanapaswa kuithinisha mchakato mzima.